0
Kipi Sijasikia - Prof. Jay (Ft. Diamond Platnumz)
0 0
Kipi Sijasikia - Prof. Jay (Ft. Diamond Platnumz)
[Verse 1: Prof. Jay]
Ah
Niliacha kazi nifanye muziki wakatabiri nitalost
Wengine wakanishawishi tuloge kuondoa mikosi
Nakomaa na muziki ingawa jua la utosi
Naamini wote tunapita na kamwe maiti haijioshi
Jina langu lishatumika sana kutajirisha watu
Nyota ndogo alishasema kuna Watu na viatu
Bunduki haiui watu ila watu ndio wanaua watu
Dunia kama jalala tazama kwa Jicho la Tatu
Ni saa mbaya watu wanahusda na roho mbaya
Tunawaita watakatifu kumbe ndio ma vampire
Yalisemwa mengi demu wangu alivyotoroka
Ni Fundisho tosha na changamoto kwa Mwanachoka
Nimepita Mengi mitihani ya kila Namna
Ndio maana mi sishangai wakiniita mbeba Lawama
Washkaji wengine fake kwenye deal hawakujui
Wanadhani kila jogoo akiwikia ni Asubuhi
Riziki hamuwezi iziba labda m'taichelewesha tuu
M'nakesha m'nishushe Mwenyezi ananipaisha
Kote milikobana kidume ndio Natusua
M'nanijua, Nakamua, roho za wangu zingaungua
Platnumz

[Chorus: Diamond Platnumz]
Oh
Unaehukumu ni wewe
Mwenyezi Mungu naomba unilinde
Kwenye hii vita milele
Nami nishike mkono nishinde
Unaehukumu ni wewe, ah
Mwenyezi Mungu naomba unilinde, ah
Kwenye hii vita milele
Mwanachoka dama nishinde
Comments (0)
The minimum comment length is 50 characters.
Information
There are no comments yet. You can be the first!
Login Register
Log into your account
And gain new opportunities
Forgot your password?