[Verse 1: Nyota Ndogo]
Nasikia wanitafuta
Kama wanipenda nakuomba njoo kwetu
Na ile njia ninayopita
Wanifatafata nakuomba njoo kwetu
Mzee Ali alinikataza kuhusu wewe
Na dadangu Aisha alinikanya kuhusu wewe

[Chorus: Nyota Ndogo]
Nalinda
Heshima yangu, Utu wangu
Moyo wangu usiumie
Nalinda
Heshima yangu, Utu wangu
Moyo wangu usiumie

[Verse 2: H_art the Band]
Nimeambiwa
Umesikia sifa zangu mbaya
Kuwa mimi kinara
Kwenye karata ya wanadada
Ukweli usemwe mama
Uzuri wako umezidi wale wote nimeona
Na usifunge moyo sana
Kwani wewe mwenyewe ndio sababu kuu mimi kupona
Nataka kukujulisha
Wewe ndio utanibadilisha
Tabia zangu nitasafisha
Mipango yote tuweze kamilisha
Mahari mi nitalipa
Kunyunyuzie penzi bila kupima
Naomba Nyota yangu ufanye hima
Usikazie moyo wako kupenda (penda)
Comments (0)
The minimum comment length is 50 characters.
Information
There are no comments yet. You can be the first!
Login Register
Log into your account
And gain new opportunities
Forgot your password?