Kama itatokea siku, utanimiss mie
Namba yangu ile ile naomba unipigie
Kama umepata muda unitembelee
Si kwa ubaya ila, hali tu unijulie

Vita vya ukimya tuliopigana mimi na wewe
Nimekiri nimeshindwa mimi bado ni yule yule
Uliugusa moyo wangu nakuleta tofauti pale
Kwenye kapu langu la hisia nafasi nyingine unipatie
Ooh, hakuna wakulijaza pengo lakooo
Moyo mtima unatamani pendo lako
Nipendwapo napajua ndio maana napajali
Maumivu yako nayatambua nimechoka kuwa mbali
Na kumiss kumiss honey wewe
Sio rahisi rahisi kuwa mwenyewe

Nipigie nipigie
Nipigie nipigie
Nipigie hata kidogo nikusalimie
Nipigie nipigie
Nipigie nipigie
Nipigie japo hali nikujuliе

Kama ukipata muda
Sauti yangu uisikie
Msimamo wangu ule ule
Kisa au sеma nirudie
Kama ukipata wasaa usinizungumzie
Si ulipata wengine mie niache usinifikirie
Sura yako maridhawa umeizalilisha
Kwa tabia yako
Niache niache baki peke yako
Moyo wangu umeugawa umenihuzunisha
Basi fanya yako
Niache niache mwana wa mwenzako
Comments (0)
The minimum comment length is 50 characters.
Information
There are no comments yet. You can be the first!
Login Register
Log into your account
And gain new opportunities
Forgot your password?